MSANII wa kundi la Ze Komedi la Eatv, Robert Augustino ‘Kiwewe’ (Pichani), anatarajiwa kuachia kazi mpya ya filamu ya vichekesho inayokwenda kwa jina la ‘My Name is Mr. Dalali’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kiwewe alisema kazi hiyo itakuwa iliyojaa visa, mikasa na matukio kibao ya Kitanzania, ambapo imechezwa kiufundi na kwa ubora wa hali ya juu, ambao umezingatia tamaduni za Kitanzania.
Kiwewe alisema katika komedi hiyo amewashirikisha wasanii nguli hapa nchini wakiwamo Mtanga, Bambo, Tin White, Ringo, Dalali pamoja na swahiba wake, Matumaini, bila kumsahu Mkono.
“Filamu ipo tayari, kilichobaki atokee msambazaji ili aiingize sokoni'