come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

PIGO LINGINE SIMBA.....

EZEKIEL Kamwaga ambaye alikuwa msemaji wa klabu ya Simba ametangaza kutoendelea tena na kazi yake hiyo na sasa anageukia taaluma yake ya uandishi wa habari, Kamwaga ameyasema hayo jana, mara baada ya mkataba wake na Simba kumalizika


Akiwa mwenye furaha na amani, Kamwaga amesema kuwa ameitumikia Simba kwa uadirifu na sasa anaangalia maisha yake binafsi, Kwa kitendo chake cha kutoendelea tena na mkataba mwingine ndani ya Simba, Kunaifanya klabu hiyo kupata pigo lingine baada ya kuondokewa na nyota wake kadhaa katika siku za hivi karibuni.

Simba imeondokewa na wachezaji wake mahiri ambao ni Mrisho Ngassa aliyetimkia Yanga, Haruna Moshi 'Boban', Juma Nyosso, huku Amri Kiemba akitajwa naye kutua Yanga, Naye mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage alinukuliwa katika kipindi cha michezo jana kuwa Kamwaga hawezi kuondoka Simba na wamepanga kumpa mkataba mwingine wa miaka miwili