come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

GOLI LA MNYATE LAING'ARISHA MWADUI, LAIPA UBINGWA YANGA SC.

Na Mwandishi wetu.

LIGI ya VodaCom Tanzania Bara leo imeendelea kutimua vumbi katika viwanja   mbalimbali, lakini Kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, timu ya Mwadui kutoka Shinyanga imeibuka na ushindi baada ya kuibabiza timu ya Simba ya Dar es salaam, goli 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji Jamal Mnyate

Kwa matokeo hayo ya leo, inamaana kwamba sasa klabu ya Yanga ndio bingwa mfululizo kwa mwaka 2015 na 2016 baada ya kufikisha pointi 68 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yoyote hata kama zitashinda mechi zao zote zilizobakia.

Simba ina pointi 58 imecheza michezo 27, imebakiza michezo matatu ambayo ikishinda yote itafikisha pointi 67. Wakati Azam yenyewe ina pointi 60 imecheza michezo 28, imebakiza michezo 2 ambayo ikifanikiwa kushinda yote itafikisha pointi 66.

Kwa maana hiyo ni wazi kabisa, goli la Jamal Mnyate Simba licha ya kuing'arisha timu yake ya Mwadui, lakini pia imeirahisishia Yanga SC kutangazwa mabingwa wakiwa na mchezo miwili mkononi.

Kikosi cha timu ya Mwadui SC kutoka Shinyanga.