.Awali, kupitia barua iliyoandikwa Machi 13, 2013 na Katibu Mkuu wa
Etoile, Adel Ghith kwenda kwa rais (mwenyekiti) wa Simba, ilielezwa
kwamba fedha za Okwi kiasi cha dola za Marekani 300,000 (Sh. milioni
480) zingelipwa ndani ya kipindi kifupi kuanzia wakati huo kwani tatizo
kubwa lilikuwa ni kupata idhini ya Benki Kuu ya Tunisia ili kukamilisha
muamala wa malipo ya fedha hizo za kigeni kwenda Simba.
Alisema mazungumzo ambayo yamefanyika wakiwa huko kuhusiana na Okwi
yamewasilishwa katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na sasa
Etoile wameahidi kutekeleza ahadi ya kulipa fedha hizo.
Hanspope aliongeza kuwa baada ya klabu yao kupata malipo hayo,
watakamilisha masuala mbalimbali ya utendaji yaliyokwama ambapo Simba
nayo ilikuwa inapata mapato ya milangoni 'kiduchu' kutokana na kufanya
vibaya kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
"Tumezungumza na kila tulichokubaliana tumekiwasilisha FIFA kwa
maandishi, wenzetu (Etoile) walijitetea kwamba mapato yao yalipungua
hivyo fedha walizokuwa wanategemea ni kupitia katika majengo ya hoteli
na maduka, ila za milangoni ambazo huwa ni nyingi hawakuwa nazo kutokana
na kucheza bila mashabiki," alisema Hanspoppe.
Wakati huo huo, wachezaji wa Simba wanaendelea na mazoezi chini ya
kocha wao mpya, Abdallah Kibadeni kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es
Salaam wakati wachezaji yosso jana walihamia kwenye uwanja wa Mwenge
Shooting wakiwa chini ya beki wa zamani wa timu hiyo, Amri Said.