|
|
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, ameapa kuwa
kikosi chake kitadhihirisha umaahiri wao watakapozuru Paris Jumatano
kwenye kombe la mabingwa baada ya kutolewa manyoya na Crystal Palace kwa
kishindo katika ligi ya Premier ya Uingereza.
Mourinho aligadhabika na viungo wake wanaolipwa maridhawa kukosa bidii baada ya kuangushwa 1-0 na Palace ambao wanangangania kubaki daraja hilo Jumamosi iliyopita.
Huku akipongeza walinda ngome wake kwa kubaki imara, Mourinho alieleza wanahabari bila ya kutaja majina kuwa kuna wachezaji wengine ambao hawashughuliki na kushamiri wakati wanapozuru vilabu visivyo maarufu.
La kuliwaza, aliendelea, ni kuwa kikosi chake kitapata msukumo wa kutamba watakapo kutana na wakwasi wa Ufaransa, Paris St Germain kwenye mkondo wa kwanza wa robo fainali ya kombe la mabingwa.
“Starehe yao ni kucheza kwenye mechi kama ya Pris. Mechi kubwa, uwanja mkuu na wapinzani wenye ubora, watakuwa sawa kwani watakuwa kwenye mazingira asili. Hiyo itakuwa mechi nzuri,” Mourinho alibeza.
Raia huyo wa Ureno anawania kuwa meneja wa kwanza kutwaa taji la mabingwa na vilabu tatu baada ya kuongoza Porto kulishinda 2004 na Inter Milan miaka sita baadaye.
Alitangaza mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto’o hatarajiwi kushiriki huku beki wa kulia, Ashley Cole hatoshiriki kamwe.