|
|
Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, amekataa
kuungana na mashabiki wa klabu chake ambao wamesisimuka na uwezekano wa
kunyakua taji la ligi ya Premier ya Uingereza licha ya kutwaa uongozi
Jumapili.
Mwalimu huyo pia alikiri ushindi wao wa 4-0 dhidi ya Tottenham Hotspurs ulikuwa wa kuchangamsha mno.
“Tulitekeleza onyesho la nguvu kutoka kipenga cha mwanzo na najivunia timu hii. Hatuna shinikizo au duku duku lolote na nina imani kubwa na jinsi vijana wangu wanavyocheza pasi na ari yao,” Rodgers alisema.
Liverpool walishinda mechi zao 18 za mwisho waliponyakua taji hilo 1990 lilipojulikana kama daraja ya kwanza lakini hawajafanikiwa kutawala tangu libadilike na kuitwa Premier.
Ikisalia mechi sita, wamesonga alama mbili mbele ya Chelsea walio nafasi ya pili huku Manchester City wakiwa wa tatu pointi nne nyuma ingawa wamecheza mechi mbili chache.
Chelsea na City watatembea nyumbani kwa Liverpool, Anfield, katika harakati za kutamatisha msimu wa sasa, uga ambao viongozi hao wamelazwa mara moja tu muhula huu.
“La muhimu ni kuwa makini na hatima yetu na linalofuata ni kuchambua West Ham na langu ni kuandaa kikosi na tuone tutafikia wapi,” Rodgers aliongeza.
Kiungo wake Jordan Henderson alichangia: "Ndoto ya kila mmoja ni kushinda kombe la Premier siku moja lakini tunastahili kumakinika na mechi inayofuata tukingoja hatima yetu mwisho wa msimu.”
Tottenham walisalia nafasi ya sita, alama nane nyuma ya waasimu wao Arsenal wanaomiliki nafasi ya nne huku meneja wao, Tim Sherwood, azimio la kufuzu kombe la mabingwa kwa kumaliza katika nafasi hio limetibuka.