come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

HUSSEIN JUMBE AJITABIRIA KIFO CHAKE.

'KILIO cha Swahiba' wimbo wa mwanamuziki mkongwe wa dansi nchini Hussein Jumbe ambaye pia ni mkurugenzi wa Talent Band yenye maskani yake jijini Dar es Salaam umeanza kurejesha upya enzi za wimbo wake wa zamani 'Nachechemea' ambao ulielezea mateso yake ya maradhi.

Wimbo mpya wa mwanamuziki huyo ambao kwa sasa unasikika kama sehemu ya kuombeleza kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Nelson Mandela, wimbo huo unatajwa kama kauli ya mwisho ya mwanamuziki huyo kutokana na ujumbe uliobeba katika mashairi yake.

Baadhi ya wapenzi wa muziki wa dansi hasa wanaoshabikia kazi ya mwanamuziki huyo wamedai Jumbe amejitabiria kifo chake mwenyewe, katika wimbo huo Jumbe ameimba kwa hisia kali huku akilalamika na mateso ya duniani, aidha Jumbe amtumia kuwaaga mashabiki wake wa Msondo Ngoma kuwa hawatamuona tena akiimba jukwaani.

Aliendelea kuimba kwa hisia na kudai Wanasikinde pamoja na wale wa bendi yake ya Talent nao hawatamuona jukwaani akiimba na tayari atakuwa ametangulia mbele ya haki, licha kwamba huo ni wimbo kama ule ya marehemu Remmy Ongala, lakini unatajwa kama maneno yake ya mwisho kabla ya kukumbwa na mauti.


STAA WA LEO ilipomuuliza Jumbe kama wimbo huo ameutunga kwa ajili yake siku atakapokufa, Jumbe alicheka na kusema, 'Huo ni wimbo kaa nyingine, nimejaribu kufikisha ujumbe mbele ya jamii kuwa mwanadamu anaweza asionekane tena kama mmezoea kumuona kwenye majukwaa', aliongeza.

Alidai kuwa yeye ni binadamu na anaweza kufa siku yoyote, lakini yeye ni mwanamuziki na ametumia kuwasilisha ujumbe kwa jamii kuwa kuna kifo tu kinaweza kukuondoa duniani na kuacha kila kitu ikiwemo familia yako.