NYOTA
wa Brazil, Neymar jana alianza kutanua mbawa zake Ulaya, baada ya
kufunga mabao matatu ndani ya dakika 13 katika ushindi wa Barcelona ya
Hispania wa 6-1 dhidi ya Celtic ya Scotland katika mchezo wa mwisho wa
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa kufanya hivyo, Neymar ameingia kwenye orodha ya wachezaji waliofunga hat trick za haraka, yaani kufunga mabao matatu ndani ya muda mfupi katika michuano ya Ulaya.
Desemba 7, mwaka jana Claudio Pizarro wa Bayern Munich
naye aliingia katika orodha ya wachezaji waliofunga hat trick za
mapema, akifunga mabao matatu dhidi ya Lille ya Ufaransa ndani ya dakika
15.
Barcelona jana licha ya kuwakosa Andres Iniesta aliyebaki benchi, Leo Messi ambaye bado majeruhi na Cesc Fabregas anayetumikia adhabu, iliichapa mabao 6-1 Celtic.
Neymar
aliyeongoza safu ya ushambuliaji hakufanya makosa baada ya kufunga hat
trick yake ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa dakika za 45, 48 na 58,
wakati mabao mengine yalifungwa na Pique dakika ya saba, Pedro dakika ya
39, na Tello dakika ya 72.
Je,
huu ni mwanzo wa Mbrazil huyo kuwasha moto zaidi Ulaya kuelekea kuwa
mfalme wa dunia, akiwapindua Ronaldo na Messi? Bila shaka hilo ni jambo
la kusubiri na kuona.
HAT-TRICKS ZA MAPEMA ZAIDI LIGI YA MABINGWA
Tarahe | Mchezaji | Timu yake | Mpinzani | Minutes |
07/12/2011 | Bafetimbi Gomis | Lyon | Dinamo Zagreb | 7 |
06/12/1995 | Mike Newell | Blackburn | Rosenborg | 9 |
25/11/1992 | Marco van Basten | AC Milan | IFK Gothenburg | 11 |
11/12/2013 | Neymar | Barcelona | Celtic | 13 |
07/12/2012 | Claudio Pizarro | Bayern Munich | Lille |