Tanzania ikiwa katika uwanja
wake wa nyumbani Taifa Stars imeshindwa kutamba mbele ya majirani zao
kutoka kusini Msumbiji baada ya kulazimishwa sare ya bao 2 - 2 katika
kuania kucheza michuano kombe la Mataifa ya Afrika.
Nchi ya Afrika mashariki iliyofurukuta ni Uganda iliyokwamisha 2 - 0 dhidi ya Mauritania.
Huko Benin, Malawi imepigwa bao 1 - 0
Bila shaka Wacongo wamekesha wakicheza muziki baada ya kuwavumishia majirani zao Rwanda kwa bao 2 - 0
Sierra Leone nao wakawabamiza ushelisheli bao 2 - 0.