come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

BATAROKOTA KUIPELEKA KWEJAGA-NYANGISHA TANGA

Na Fikiri Salum

WASANII wa muziki wa hip hop Batarokota Linda ambaye alikuwa mshiriki wa tuzo za kilimanjaro music award 2014 atapanda jukwaa moja na mwanaharakati Mkola Man katika jiji la Tanga wakati wa sikukuu ya Idd mosi.

Akizungumza na ukurasa huu, Batarokota aliyekuwa ziarani Zanzibar, amesema anatarajia kuwasili Tanga mapema kabla ya sikukuu tayari kujiandaa na shoo hiyo.

'Ni kweli nimepata mwaliko kutoka Tanga na nitafanya shoo siku ya sikukuuu ya Idd mosi, nitaimba nyimbo zangu zote za zamani pamoja na ule ulioshindanishwa katika tuzo za Kill mwaka huu 'Kwejaga-Nyangisha', alisema.


Msanii huyo ambaye ni mpole lakini akishika maiki huwa kichaa amedai muziki upondani ya damu yake, licha ya kushindanishwa katika kipengele cha muziki wa asili,  Batarokota ni mwana hip hop na ataachia nyimbo zake alizorekodi akichana mistari kama 2Pac.'Wengi wananijua kwa muziki wa asili, lakini mimi naimba hip hop' alisema.