come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

UMOJA NI NGUVU MABINGWA CARLOS CUP

Timu ya Umoja ni Nguvu ya Usagara mkoani Tanga (Pichani), imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Carlos Power Cup baada ya kuilaza timu ya Pentagon pia ya Usagara kwa mabao 5-4 kwa njia ya matuta baada ya kushindwa kufungana kwa muda wa dakika 90.


Kwa mujibu wa muandaaji wa mashindano hayo Carlos Hiza amesema kuwa michuano yake imemalizika salama na timu ya Umoja ni Nguvu kutwaa ubingwa ambapo ameikabidhi jezi pamoja na kombe, Pia timu ya Mtotesho imeweza kukamata nafasi ya tatu.

Akielezea mechi ya fainali, Hiza alidai kuwa mechi ya fainali ilikuwa ngumu ambapo muda wote mashabiki walishuhudia burudani safi toka kwa timu zote mbili, Muda wa kawaida ulipomalizika timu zilienda kwenye mikwaju ya penalti tano tano ambapo ushindani pia uliweza kuonekana.

Umoja ni Nguvu ilipata penalti zote tano huku wenzao wa Pentagon pia walipata penalti tano na kuongezwa nyingie mbili mbili ambapo Pentagon walikosa moja huku wenzao wa Umoja ni Nguvu walipata zote na kuibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo iliyotimua vumbi katikia viunga vya Tanga.

Michuano mingine iko tayari na muda wowote inaweza kuanza, Carlos Hiza ni diwani wa Usagara kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM