MTANDAO wa Mambo Uwanjani unaomilikiwa na Prince Hoza ambao umefikisha mwaka mmoja tangia kuanzishwa kwake umeweza kung'ara hasa kutokana na idadi kubwa ya wasomaji wake ndani na nje ya Tanzania.
Hadi sasa mtandao huo umetazamwa na watu wasiopungua milioni moja huku nchi za Tanzania, Marekani, Uingereza na Uholanzi zikiongoza kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi duniani.
Nchi ya Kenya inafuatia kwa ukanda wa Afrika mashariki wakati India inaongoza kwa upande wa bara Asia, takwimu hizo zilizotolewa kufuatana na mpangilio wa utazamwaji wa mtandao huo wa habari unaonyesha kuwa nchi za Ulaya na Amerika ndizo zenye watazamaji wengi zaidi.
Msanii Nasseb Abdul maarufu Diamond Platinum na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda Moses Oloya ndio vinara kwa kujizolea wasomaji lukuki ambao wamekuwa wakizisoma taarifa zao.
1-Diamond Platinum
Diamond anaongoza kwa kusomwa zaidi huku akifuatiwa na mchezaji Moses Oloya ambaye alijipatia wasomaji wengi wakati anataka kusajiliwa na vilabu vya Simba na Yanga.
2-Moses Oloya anakamata nafasi ya pili, habari zake za kuwaniwa na vilabu vya Simba na Yanga zilimwezesha kutazamwa na idadi kubwa ya watu na kumfanya ashike nafasi hiyo.
3-Meneja wa kundi la sanaa la Super shine Modern Taarab Kais musa Kais anakamata nafasi tatu, Kais ameingia katika kundi la watu maarufu wanaotazamwa sana kutokana na kufiwa na mke wake Nyawana Fundikira ambaye alikuwa mtangazaji na mwimbaji wa taarabu.
4-Vifo vya wanajeshi saba wa Tanzania huko Darfur Sudan vimeingia katika orodha ya taarifa gumzo zaidi katika mtandao huo, wanajeshi hao waliuawa katika mlipuko wa bomu uliofanywa na waasi huko Darfur.
5-Mlinda lango Juma Kaseja ambaye alitemwa na timu yake ya Simba naye alipata umaarufu na kuandikwa sana mitandaoni, Kaseja alikuwa akimulikwa na vilabu mbalimbali ambapo vilitaka kumsajili, timu ya Mtibwa Sugar ndio iliyotaka kumsajili ambapo taarifa zake ziliandikwa na mtandao huu na kutembelewa na watu wengi.
6-Mwanamuziki aliyejitangaza ni mfuasi wa Freemason mwenye maskani yake jijini Tanga Mkola Man aliingia katika nafasi hiyo huku habari zake zikitazamwa na watu wengi.
7-Tamasha la Simba Day ambalo huandaliwa na klabu ya Simba lilikamata nafasi ya saba huku wachezaji Mrisho Ngasa na Moses Oloya wakitangazwa kutambulishwa katika tamasha hilo, Oloya alikuwa akitakiwa na Yanga huku Ngasa tayari alishatangazwa na Yanga kama mchezaji mpya.
8-Sakata la mshambuliaji wa Liverpool ya England Luis Suarez nalo liliweza kukonga vichwa vya habari mbalimbali duniani, Suarez amekamata nafasi ya nane katika mtandao huo.
9-Mtangazaji wa kipindi cha michezo cha redio Clouds Shaffih Dauda naye amechomoza hadi nafasi ya tisa, kupingana kwake na TFF iliyokuwa chini yake Leodegar Tenga kulipelekea kushutumiwa vikali na ndipo habari zake zilipopata kutazamwa sana.
10-Mshambuliaji na mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo anayekipiga Real Madrid ya Hispania alitajwa mapema kama atachukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia
.Ronaldo alikuwa akipewa nafasi kubwa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika klabu yake na timu ya taifa ya Ureno iliyofuzu kwa fainali za kombe la dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwaka huu.
AZUNGUMZIA MAENDELEO YA BLOGU YAKE
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkurugenzi wa Mambo Uwanjani Publishers ambao ndio wamiliki na watayarishaji wa blogu hiyo Prince Salum Hoza ambaye pia ni mwandishi wa habari amesema bado jitihada zinaendelea ili kufikia malengo.
'Malengo yangu kuifanya blogu hii iwe ya Watanzanjia wote bila kujali itikadi wala nini, hii ni blogu ya kijamii hakuna Usimba wala Uyanga pia itikadi za kisiasa tumeziweka kando', alisema na kuongeza
.'Masuala ya kupendelea CCM, Chadema au CUF hapa hilo hakuna isipokuwa tunajali uzalendo, pia hatuna ubaguzi wa kidini, rangi wala jinsia tunazipa umuhimu habari zote', aliongeza.
Kuhusu idadi ya waandishi wanaotumikia Mambo uwanjani blogspot, Hoza amedai mpaka sasa hakuna idadi kamili ya waandishi kwakuwa bado changamoto zinaendelea.'Kwa sasa nina waandishi wasiopungua wanne ambao ni Exipedito Mataruma, Elias John, Regina Mkonde, Salum Fikiri na mimi mwenyewe', aliongeza.
MATARAJIO YA BAADAYE
Hoza amesema malengo yake yatakamilika endapo blogu yake itapata matangazo ya kutosha, anamshukuru mdhamini wake Chifu Panduka na Angaza House Agent ambao wamekuwa wakimwezesha mara kwa mara, pia anawashukuru wadau wote ambao wamekuwa watazamaji wazuri na kumpa nguvu.
Kuhusu maendeleo mengine amesema mpaka sasa kampuni yake inamiliki blogu mbili ambazo ni Mambo uwanjani blogspot na Staa wa leo, aidha Hoza ameongeza kuwa ana mipango ya kuanzisha gazeti lake la michezo kwa lengo la kuzipa sapoti blogu zake