come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

KATIKA WACHE3ZAJI YANGA, JAVU AMEONYESHA UWEZO

Na Fikiri Salum

MSHAMBULIAJI Hussein Javu ambaye alisajiliwa mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Manungu Tuliani wilayani Mvomero mkoani Morogoro ni mmoja kati ya wachezaji wa Yanga walioonyesha uwezo mkubwa kwenye ligi kuu Tanzania bara iliyomalizika hivi karibuni.

Kwa mujibu wa tkwimu zetu, Javu ni miongoni mwa wachezaji wanaostahili kusalia katika kikosi hicho kilichokamata nafasi ya pili nyuma ya mabingwa wapya Azam fc.

Ingawa nafasi hiyo imeonekana kuwakera wapenzi na mashabiki wa Yanga msimu huu kwakuwa umeweza kuwanyang'anya ubingwa waliokuwa wakiushikilia.


Yanga ilimaliza ligi mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo ilipambana na mahasimu wake wakuu Simba na kutoka sare ya kufungana 1-1 hivyo kuhitimisha ligi katika nafasi ya pili ikiwa imefikisha pointi 57.


Mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu bara kocha mkuu wa Yanga Mholanzi Hans Van Der Pluijm anatarajia kuwasilisha ripoti kamili ya kikosi hicho kwa kamati ya utendaji ya Yanga, ripoti hiyo itabainisha uwezo binafsi wa mchezaji mmoja mmoja na wapi walipokosea.

Kocha ataweka msimamo wake kama anahitaji wachezaji wa aina gani huku akipendekeza kuachwa kwa baadhi ya wachezaji ambao hawakuonyesha viwango vinastahili kuichezea Yanga.Msimu uliopita Yanga ilitwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania  bara ikiwa chini yake Mholanzi mwingine Ernie Brandts akisaidiana na Fred Minziro, makocha hao walitimuliwa mwezi

Desemba mwaka jana kufuatia kipigo cha 3-1 dhidi ya Simba.Licha ya Yanga kufanya usajili mkubwa uliogharimu mamilioni ya fedha bado imeshindwa kutetea ubingwa wake msimu huu ukichukuliwa kwa mara ya kwanza na 'Wanalambalamba' Azam fc yenye maskani yake Chamanzi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Yanga iliamua kufanya usajili wa nguvu kwa lengo la kuimarisha kikosi chake kujiandaa na michuano ya klabu bingwa barani Afrika pamoja na kutetea taji lao la ligi kuu bara, kikosi hicho kilikwenda kuweka kambi yake nchini Uturuki.

Nyota muhimu kama Juma Kaseja kipa aliyepata kuitwa Tanzania One kutokana na uhodari wake wa kuzuia michomo, mshambuliaji hatari raia wa Uganda Emmanuel Anord Okwi, winga Mrisho Ngasa, kiungo Hassan Dilunga, Hussein Javu, Shaaban Kondo, Reliant Lusajo na wengineo lakini bado wameshindwa kutetea ubingwa wao msimu huu huku wakiondoshwa mapema kwenye ligi ya mabingwa Afrika.

Kushindwa huko kwa Yanga kusonga mbele katika ligi ya mabingwa msimu huu na kutetea ubingwa wao kumepelekea simanzi kwa Wanayanga ambao waliamini uwepo wa nyota hao ungeweza kuisaidia timu yao.

Wapo wachezaji walioshindwa kuisaidia Yanga katika mechi muhimu na kusababisha kuandamwa na baadhi ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo, tuhuma kwao zilianza pale Yanga ilipoonekana kufanya vibaya hata kama ilionyesha uwezo mkubwa uwanjani.

Kikosi cha Yanga msimu huu kilionekana dhahiri kutisha timu pinzani kutokana na matokeo mazuri iliyokuwa ikiyapata katika mechi zake, Ushindi mnono wa mabao 7-0, 5-0 ulikuwa chachu muhimu kwa timu hiyo kufanya vizuri.

Lakini kwa mshangao mkubwa Yanga ilipoteza katika mechi zake muhimu ambazo ingetumia vema nafasi ilizopata kwa vyovyote ingestahili ubingwa, katika ligi ya bara Yanga itaweza kujutia mechi zake tatu ambazo ni dhidi ya Mtibwa Sugar, Azam fc na Mgambo JKT.

Safu ya ushambuliaji ilionekana kupwaya, lakini mwalimu wa timu hiyo alipoanza kumtumia Hussein Javu matunda yake yalianzakuonekana, Javu kwa kutumia uzoefu wake aliokuwa nao tangia akiwa Mtibwa Sugar alianza kufufua matumaini ya ubingwa kwa klabu yake ya Yanga.

Mshambuliaji huyo aliweza kushirikiana vema na wenzake na kuitakatisha safu ya ushambuliaji ya Yanga, ni mmoja wa wachezaji wanaostahili kusalia katika klabu hiyo kwani huenda akawa mwiba smimu ujao. Ligi ya msimu ujao nyota wa kigeni watakaoruhusiwa ni watatu tu badala ya watano, hivyokwa vyovyote Yanga itasaliwa na washambuliaji wake wawili na mlinzi mmoja,

Javu anaweza kuwa msaada muhimu katika klabu ya Yanga.Amejitahidi katikamechi zake chache alizocheza ikiwemo ile na mtani wa jadi Simba, kuingia kwake kuliweza kuleta changamoto iliyopelekea Yanga kupata bao la kusawazisha lililowekwa kimiani na Simon Msuva.

Simpigii debe Javu ili asitemwe ila kila shabiki ameona uwezo wake, Javu alikuwa muhimu kwenye mechi za ugenini ilizocheza Yanga ambazo zilionekana kuwa na ushindani mkubwa.Javu anakumbukwa alipowahi kuiliza Yanga katika mchezo wa ligi kuu alipokuwa anaichezea Mtibwa Sugar, katika mchezo huo Yanga ililala mabao 3-0 mawili yakiwekwa kimiani na Javu huku lingine likifungwa na Awadh Juma ambaye kwa sasa amejiunga na Simba.

Uongozi wa Yanga unapaswa kuheshimu matakwa ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa timu yao ili kuweza kufanya usajili makini utakaoweza kuleta tija kwa klabu yao, Yanga inapaswa kuachana na wachezaji wenye majina makubwa ambao hufuata maslahi na si mapenzi kama ilivyo kwa wasio na majina.

Nina imani mchezaji kama Javu anahitaji muda ili awewe kuonyesha kiwango chake, najua makocha wa Yanga wanafurahishwa na uwezo wake hivyo nafasi watakayompa itatumiwa vema na kuipa faida kubwa Yanga, mwakani Yanga itashiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.