Mtayarishaji na msanii wa muvi za kibongo anayetesa kupitia filamu zake mbalimbali Nelly Kim 'Sibonike' anatarajia kuachia filamu yake nyingine iitwayo 'Word of God' hivi karibuni.
Akizungumza na mtandao huu leo, Sibonike (Pichani) amedai kuwa muvi yake hiyo ina maudhui ya kimungu na inafundisha jamii ya Kitanzania ambayo imeelekea kupoteza mwelekeo.
Amedai kwamba ndani ya muvi hiyo amewashirikisha nyota kadhaa ambao wamechangia kwa namna moja au nyingine kuing'arisha, Aliwataja mastaa hao kuwa ni pamoja na Kajala Masanja, Benny Branco, Fatuma Makongoro 'Bi Mwenda',
Mohamed Fungafunga 'Jengua', Lumole Matovolwa 'Big', Pastor Jimmy Mafufu, Tecra Mjata.
Wengine ni Hashim Kambi 'Kambi', Elia Daniel 'Elly G'na wengineo.
Muvi hiyo itatoka hivi karibuni ikiwa chini ya kampuni yake mpya ya Kasinge Production, Sibonike amewahi kushiriki filamu mbalimbali ikiwemo ya 'Becouse of You', The Devils Kingdom, Morning Alarm, Riple of Tears na Desepction, filamu hizo alizicheza kupitia kampuni ya marehemu Steven Kanumba 'The Great'.