come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Beckham kuchomoa tawasifu mpya

David Beckham

Nahodha wa zamani wa Uingereza David Beckham atachomoa tawasifu yake ya hivi karibuni zaidi mwezi Oktoba kupitia mkataba na kitengo cha uchapishaji kutoka Uingereza cha kampuni ya Ufaransa Lagardere.

Kiungo huyo wa kati wa zamani wa Manchester United na Real Madrid, aliyestaafu kutoka soka Mei baada ya kukaa muda mfupi katika klabu ya Ufaransa Paris St Germain, anatarajiwa kuchomoa tawasifu yake ya nne Oktoba 31 kupitia Headline Publishing Group yenye makao yake Uingereza na inayomilikiwa na Lagardere.
Mkurugenzi wa Headline wa vitabu visivyo vya kubuni, Jonathan Taylor, alinunua haki za kuchapisha kitabu hicho duniani kupitia mkataba na kampuni ya XIX Entertainment inayosimamia masuala ya mchezaji huyo wa umri wa miaka 38. Mchapishaji huyo alisema kitabu hiyo kitakuwa cha kutoa heshima kwa enzi ya uchezaji ya nyota huyo.
"David Beckham ni, bila shaka yoyote, mchezaji anayekubalika kote na anayetambuliwa duniani, na kitabu hiki kitakuwa njia mwafaka zaidi kwa mamilioni ya mashabiki wake duniani kusherehekea ufanisi wa David katika soka,” Taylor alisema kupitia taarifa.
Beckham alichezea Uingereza miaka 115, ambayo ni rekodi kwa mchezaji wa katikati ya uwanja, na alishinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, mataji sita ya Ligi Kuu ya UIngereza na mawili ya FA akiwa na Manchester United.
Pia alishinda mataji akiwa na Real Madrid nchini UHispania, LA Galaxy Marekani na PSG Ufaransa.
Kitabu hicho chake kipya ni sehemu ya mipango ya baada ya kustaafu ya mchezaji huyo tajiri zaidi Uingereza, ambaye umashuhuri wake na sifa zake kama mwanamume wa familia zinafaa kumhakikishia kuwa nembo ya Beckham inaendelea kunawiri.
Beckham ambaye husimamiwa na XIX Entertainment ambayo pia husimamia mwendeshaji magari wa Uingereza Lewis Hamilton na bingwa wa tenisi wa Wimbledon Andy Murray ametumia sura yake ya kifilamu na mwili wake wa kimichezo kutangaza suruali za ndani zinazotengenezwa na kampuni ya mavazi ya H&M kutoka Sweden na saa za kampuni ya Breitling kutoka Uswizi.
Ameoa Spice Girl wa zamani aliyegeuka mwanamitindo wa mavazi Victoria Beckham, na wamejaliwa watoto wanne.
Lagardere ilishuhudia kuongezeka kwa asilimia 2.3 kwa mauzo yake ya robo ya kwanza Mei, jambo lililochangiwa na vitabu vilivyouzwa sana vya "Fifty Shades" na wasifu wa mchezaji nyota wa soka kutoka Sweden, Zlatan Ibrahimovic.