come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

JACK WILSHERE AIGOMBANISHA NCHI YAKE NA ENGLAND

KIUNGO Jack Wilshere amesababisha tena mgogoro baina ya klabu yake na nchi yake, England baada ya kuumia kifundo cha mguu akiichezea timu ya taifa dhidi ya Ujerumani.

Uamuzi wa kumchezesha Wilshere juzi usiku umeiudhi Arsenal, kwa sababu kocha Arsene Wenger aliomba mapema kiungo wake achezeshwe katika mechi moja tu kati ya mbili za kimataifa.

Lakini akitoka kucheza dhidi ya Chile Ijumaa usiku, akitimiza dakika 71, Wilshere pia aliingia akitokwa benchi dakika ya 64 wakati England ikifungwa 1-0 na Ujerumani na akaumia kifundo cha mguu.

Hii si mara ya kwanza Wilshere anakuwa ishu baina ya Arsenal na FA, kwani iliwahi kutokea pia wakati anachezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 kwenye michuano ya Ulaya mwaka 2011, ingawa suala hilo lilipatiwa ufumbuzi.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 pia ameelezea wasiwasi wake wa kukosa nafasi kwenye kikosi cha England kitakachokwenda kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani Brazil.