BAADA
ya kukamilikkwa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya, joto liliopo
ni je klabu nne za England zilizofuzu zitakutana na timu gani katika
hatua ya mtoano, inayojumuisha timu 16.
Kuelekea
droo hiyo Jumatatu mjini Nyon, STAA WA LEO imetabiri timu ambazo
zinaweza kukutana na klabu hizo za England katika michuano hiyo.
Mbwa mkali zaidi: Cristiano Ronaldo atataka kuboresha rekodi yake ya mabao aliyoanza nayo katika hatua ya makundi akiwa Real Madrid
Baada
ya kuangukia katika nafasi ya pili kufuatia kipigo cha Napoli jana
katika mchezo wa mwisho, Arsenal sasa inatarajiwa kuangukia kwa mpinzani
mgumu kwenye hatua hiyo ya mtoano.
Droo
huwa inazingatia mambo kadhaa kama timu kutokutana na mpinzani
iliyokuwa naye kundi moja na pia timu za nchi moja kutokutanishwa, huku
timu zilizoongoza makundi zikicheza mechi za marudiano za mtoano
nyumbani.
Hiyo inamaanisha hakuna klabu za Ligi Kuu ya England zinazoweza kupambanishwa, lakini iko wazi The Gunners na Manchester City watakutana na wapinzani wagumu baada ya kushika nafasi za pili kwenye makundi yao.
Anapambana kuwa fiti: Lionel Messi atarajea kutoka kwenye majeruhi kuiongoza Barcelona katika hatua ya mtoano
Timu zote zinatazamiwa kutoepuka kukutana na vifofo wa Hispania, Real Madrid na Barcelona, wakati timu ya Arsene Wenger inaweza kukutana na mabingwa watetezi, Bayern Munich - City haiwezi kukutana na Bayern lakini inaweza kukutana na washindi wa pili wa msimu uliopita, Borussia Dortmund.
Kwa
Chelsea na Manchester United - ratiba ngumu kwao itakuwa ni kukutana na
AC Milan. Pamoja na hayo, timu mbili zilizoongoza makundi zitapata timu
hafifu kidogo katika hatua ya mtoano.
ARSENAL
Real Madrid
PSG
Bayern Munich
Atletico Madrid
Barcelona
PSG
Bayern Munich
Atletico Madrid
Barcelona
CHELSEA
Bayer Leverkusen
Galatsaray
Olympiakos
Zenit St Petersburg
AC Milan
Galatsaray
Olympiakos
Zenit St Petersburg
AC Milan
MANCHESTER CITY
Real Madrid
PSG
Dortmund
Atletico Madrid
Barcelona
PSG
Dortmund
Atletico Madrid
Barcelona
MANCHESTER UNITED
Galatasaray
Olympiakos
Schalke
Zenit St Petersburg
AC Milan
Olympiakos
Schalke
Zenit St Petersburg
AC Milan