come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MASIKINI JUMA KASEJA, DIDA SASA NAMBARI ONE JANGWANI.

MAISHA ya kipa mwenye heshima kubwa hapa nchini Juma Kaseja sasa yapo shakani katika klabu ya Yanga kufuatia kuwekwa benchi mechi mbili mfululizo za mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara huku kipa mwenzake Deogratus Munishi 'Dida' akitangazwa rasmi kuwa Jangwani One.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinasema Kaseja ni kipawa akiba yaani namba mbili huku Ally Mustapha 'Barthez' akiwa jukwaani tu, Dida ameonyesha kiwango kizuri katika mechi mbili alizocheza hivi karibuni ambapo moja alianza na Ashanti United nyingine dhidi ya Coastal Union.

Kuhusu kuwekwa benchi kwa Kaseja, inadaiwa hakutokani na kufungwa magoli ya kizembe na Simba wakati Yanga ikilala goli 3-1 kwenye mechi ya kirafiki iliyojulikana kama 'Nani Mtani Jembe iliyochezwa Desemba 21 mwaka jana.


Taarifa zaidi zinafafanua kuwa Dida ameonyesha kumkuna kocha wa kikosi hicho Mholanzi Hans Van Der Pluijm, kocha huyo maefurahishwa na udakaji wa Dida hivyo ataendelea kumtumia katika mechi mbalimbali za ligi kuu bara, Yanga itaingia tena uwanjani siku ya jumapili kukwaana na Mbeya City