come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

NORWICH,NEWCASTLE ZASHITAKIWA ENGLAND.

Norwich City na Newcastle United zimeshtakiwa na Shirika la Soka la Uingereza, kufuatia makabiliano yaliyozuka kati ya Bradley Johnson na Loic Remy wakati wa mechi ya Ligi ya Premia wiki jana.

"Wote wawili, Norwich City na Newcastle United, wameshtakiwa na FA kwa kutohakikisha kwamba wachezaji wao wana nidhamu uwanjani na wanajizuia kuchokoza au kuzua makabiliano,” FA ilisema kupitia taarifa Jumatatu.

Mashtaka hayo yanahusiana na kisa kilichohusisha Remy wa Newcastle na Johnson wa Norwich ambapo wote wawili walisukumana kabla ya Remy kuonekana kuinamisha kichwa chake kumwelekezea Johnson karibu na mwisho was are yao ya 0-0.

Wachezaji kutoka kwa timu zote mbili waliingilia mfarakano huo kabla ya Remy na Johnson kufukuzwa uwanjani.


Johnson alibahatika na kufanikiwa kubatilisha marufuku yake baada ya kukata rufaa lakini Remy kwa sasa anatumikia marufku yake ya kutocheza mechi tatu.

Klabu hizo zina hadi Jumatano kujibu mashtaka hayo.