.Mshambuliaji kigezo wa West Ham United, amelalamikia uamuzi wa shirisho la kandanda Uingereza, FA, la kukataa kuondoa kadi yake nyekundu aliyolishwa wikendi iliyopita kwenye mechi dhidi ya Swansea.
Caroll ambaye amechezea Uingereza, atatumikia marufuku ya mechi tatu kufuatia kukataliwa kwa rufaa yake kufuatia kuondolewa uwanjani badala ya kukabiliana na mlinda ngome wa Swansea, Chico Flores.
Tukio hilo lilizua mjadala pale Flores alipoonekana kuigiza kuumia kwake pale mkono wa Caroll ulipoonekana kumgusa utosini.
Licha ya meneja wake aliyefutwa Jumanne, Michael Laudrup, kuungana na wengine haswa msimamiszi wa West Ham, Sam Alladyce, kukashifu uamuzi huyo, kamati ya kusikiza rufaa katika FA ilikubaliana na uamuzi wa refa na kukataa kubatilish kadi hiyo.
Huku West Ham wakingangana kujiondoa katika nafasi za kushuka daraja kwenye ligi ya Premier, kukosa huduma za Caroll ambaye alirejea mchezoni majuzi baada ya kuugua tangu mwanzo wa musimu ni pigo kuu.
Tangu Caroll arejee, amebuni mabao matatu na kuwezesha West Ham kushinda mechi zao mbili za mwisho na mhsmbuliaji huyo aligeukia mtandao wa kijamii wa Twitter kueleza kukerwa kwake.
“Aibu,” alindika katika anwani yake ya Twitter baada ya FA kukataa rufaa iliyowasilishwa na klabu chake.