TIMU ya Real Madrid imezifikia kwa pointi Barcelona na Atletico kileleni mwa La Liga kufuatia ushindi wa mabao 3-0 jioni ya leo dhidi ya Getafe.
Walipata bao lao la kwanza dakika ya tano kupitia kwa Jese aliyeiwahi pasi ya Bale na kumtungua kipa Miguel Angel Moya wa Getafe.
Karim Benzema akafunga bao la pili dakika ya 27 kabla ya Luka Modric kumaliza kazi dakika ya 66. Real sasa imetimiza pointi 60 sawa na Barca na Atletico, baada ya kila timu kucheza mechi 24. Barca ipo kileleni kwa sababu ina mabao 52 zaidi, Real 44 zaidi na Atletico 43