come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SUAREZ AZIDI KUING'ARISHA LIVERPOOL

Luis Suarez

Liverpool waliendelea na harakati zao za kuzoa ligi ya Premier ya Uingereza Jumamosi pale walipogeuza kufungwa kwanza na wenyeji Cardiff kuwa adhabu kali ya 6-3 wakiongozwa na nyota wao Luis Suarez aliyezamisha magoli matatu au kwa kimombo, hat-trick.

Vijana wa Brendan Rodgers walijipata nyuma ya Cardiff wanaopigania uhai wao kwenye ligi hiyo katika kipindi cha kwanza kabla kuwabwaga wakaaji wa uwanja wa Cardiff City Stadium na onyesho lingine la mashambulizi mazito.

Straika huyo wa Uruguay sasa ana mabao 28 katika shindano hili msimu huu huku Liverpool wakifunga mara 18 katika mechi tano za mwisho kuendeleza matumaini ya kunyakuwa ubingwa wa Uingereza kwa mara ya kwanza tangu 1990.

Mlinda ngome Martin Skrtel alichangia mawili, huku mshambuliaji mwenza, Daniel Sturridge akiongeza jina lake katika orodha ya mabao kudhibiti nafasi ya pili alama nne nyuma ya Chelsea waliocharaza Arsenal 6-0 katika mechi ya awali.


Cardiff walitishia mshtuko pale mabao ya Jordan Mutch na Fraizer Campbell yalipowapeleka kifua mbele katika awamu ya ufunguzi kabla ya Mutch kupata lake la pili baadaye kipindi cha pili lakini walisalia wa pili kutoka mwisho na alama tatu nyuma ya nafasi ya mwisho ya usalama.

Mutch alifungua mafuriko ya mabao dakika ya tisa pale aliposukuma mkwaju rojo rojo wavuni kutoka hatua 15 uliolemea kipa wa Liverpool, Simon Mignolet, lakini wageni walisawazisha dakika nane baadaye kupitia Suarez aliyezika krosi ya Glen Johnson kimyani.

Dakika chache baadaye, ngome ya Liverpool upande wa kulia ilipatikana usingizini pale Campbell alipokata boli ndani na kuachilia kombora la guu la kushoto kumbwaga Mignolet kufanya mambo 2-1.
Skrtel alisawazisha dakika ya 40 kwa kichwa pale alipovamia krosi ya Phillipe Courtinho kutoka hatua chache kabla ya kuwapa Liverpool uongozi kwa mara ya dakika nane baada ya kipindi cha pili kuanza pale alipotinga kutoka kona ya Courtinho.

Suarez alifunga lake la pili dakika ya 61st baada ya kupokea mpira kutoka Sturridge aliyemlisha na pasi ya kisigino kabla ya straika huyo wa Uruguay kulipisha dakika kumi baadaye kwa kumuunganishia mwenzake wa Uingereza kutia kizimbani la tano.

Mutch alifungia wenyeji la tatu dakika mbili zikisalia kabla ya Suarez kufunga udhia na kukamilisha ushindi wa 3-6 katika muda wa ziada.