Kocha wa Paris Saint Germain, Laurent Blanc alisema hadharani kuwa klabu hiyo ya Ufaransa inatamani kumsajili mshambuliaji huyo Eden Hazard.
Lakini mtandao wa Sportmail alhamisi iliyopita ulitoa taarifa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji yuko katika harakati za kusaini mkataba mpya wa miaka mitano katika klabu yake ya Chelsea na atakuwa analipwa paundi laki mbili kwa wiki.
Hazard kwasasa anajiandaa kuiwakilisha Ubelgiji kwenye fainali za kombe la dunia 2014 nchini Brazil.
'Nibakia Chelsea, nina asilimia 100`, alisema nyota huyo mwenye miaka 23.
`Kiukweli katika mpira huwezi kujua, lakini nipo chini ya mkataba na Chelsea na nataka kukaa pale`.
"Nipo katika mazungumzo ya mkataba mpya na Chelsea, Mazungumzo ndio kwanza yanaanza, lakini bado tuna muda".
"Lakini ukweli ni kwamba, Chelsea wamenipa ofa ya mkataba mpya ambao utanifanya nijiamini zaidi, kwamba nitafanya kazi nzuri zaidi na watanifurahia".
Hazard yuko mbioni kuanza kula mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki katika mkataba mpya na Chelsea
Laurent Blanc anataka kumsajili Hazard katika klabu yake ya Paris Saint-Germain majira ya kiangazi.