WACHEZAJI na viongozi wa Yanga wametoa tamko na kutoboa siri ya kushindwa kupata ushindi katika mechi zake mbili ilizocheza hivi karibuni na kuambulia pointi mbili, wachezaji wa Yanga wakiunghwa mkono na viongozi wao wamedai wanapocheza mechi na timu moja uwanjani lakini timu nyingine mbili nazo zinashiriki kupambana nayo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa Yanga wamesema wanakamiwa sana na timu pinzani lakini nje ya uwanja kuna timu nyingine mbili zinashiriki kupambana nao, Mrisho Ngasa kiungo mshambuliaji wa Yanga ametoboa siri mara baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri kila timu wanayokutana nayo kwenye ligi kuu bara imeonyesha kuwapania.
Ngasa amedai mbali na kuwapania, timu nyingine mbili ziko nje ya uwanja zikishiriki kuwahujumu, mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakuwa tayari kulitaja jina lake ameunga mkono kauli ya wachezaji na kudai Simba na Azam ndio wachawi wao nje ya uwanja na wamekuwa wakizisaidia timu nyingine inazocheza nazo.
Hata mechi yao dhidi ya Mtibwa, ambapo Yanga iliambulia ponti moja, Azam na Simba zilikuwa zikishabikia matokeo hayo ili waupoteze ubingwa wao na kukjosa nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa mwakani, lakini uongozi wa Yanga umeweka bayana kuwa msimu huu watachukua ubingwa iwe isiwe.
Uongozi umeweka wazi kilakitu kuwa Azam nayo itakwama katika mechi zake sita zilizosalia kwani timu watakazokutana nazo zina nafasi ya kutaka kujinusuru kushuka daraja huku nyingine zikitaka nafasi mbili za juu ambapo Mbeya City ni kikwazo cha Azam, ulisema uongozi