Robin van Persie alifunga mabao
matatu na kuisaidia mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza
Manchester United, kujikatia tiketi ya kushiriki robo fainali ya kombe
la kilabu bingwa
barani Ulaya baada ya kuinyuka Olympiakos mabao 3-0 katika mechi ya mkondo wa pili iliyochezwa Old TraffordMabao hayo ya Van Persie yalinusuru kocha David Moyes shtuma ya kuiumbua sifa ya ya timu hiyo ambayo imekuwaikishuhudia msururu wa matokeo duni katika ligi ya nyumbani.
Van Persie alifunga mkwaju wa penalti baada ya kuchezewa vibaya mda mchache tu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Baadaye mshambulizi huyo wa Uholanzi aliongeza bao lingine baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa mshambulizi mwenza Wayne Rooney.
Van Persie alisajili bao lake la tatu kupitia mkwaju wa free kick na kumhakikishia Moyes fursa ya kujiunga na Chelsea katika hatua ya robo fainali ya mchuano huo wenye kitita kikubwa zaidi barani Uropa.
Licha ya mashambulizi kadhaa Olympiacos kutoka Ugiriki mlinda lango wa Manchester United David De Gea alilazimika kufanya kazi ya ziada kuinyima klabu hiyo kutoka Ugiriki bao moja tu la ugenini
Olympiacos ilishinda mechi ya mkondo wa kwanza mabao 2-0 na ilihitaji sare ya aina yeyote ama bao moja tu la ugenini ilikufuzu kwa hatua ijayo kutokana na sheria ya bao la ugenini.
Timu hiyoitajilaumu yenyewe kwani ilpoteza nafasi nyingi tu za kufunga bao hilo muhimu.
Joel Campbell ambaye anaichezea kwa mkopo kutoka Arsenal alimchenga mlinzi Phil Jones akampigia pasi Hernan Perez ambaye aliboronga na kuupiga nje.
Kutokana na ushindi huo mkubwa ,Manchester United sasa inajiunga na Chelsea kama wawakilishi wa uingereza katika robo fainali .
Ujerumani inawakilishwa na mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern Munich na Borussia Dortmund huku Uhispania ikijivunia timu tatu yaani , Real Madrid, Athletico Madrid na Barcelona .
Paris Saint Germain ndiyo timu ya pekee kutoka Ufaransa.
Droo ya robo fainali ya mchuano huu itafanyika Ijumaa .