come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ASTON VILLA KUPIGWA BEI



Mmiliki wa klabu ya soka inayocheza Ligi Kuu ya Uingereza Aston Villa, Mwamerika Randy Lerner, ametangaza kwamba atauza klabu hiyo baada ya msimu mwingine wa kusikitisha wa mabingwa hao wa zamani wa Ulaya.

Lerner, aliyekuwa mmiliki wa awali wa timu ya NFL ya Cleveland Browns, alichukua umiliki wa Villa 2006 lakini alisema amechoshwa na mahangaiko ya klabu hiyo kutokana na majeraha na uvumi uliotanda majuzi kwamba alipanga kuiuza.

"Sasa wakati umefika kwangu kutafuta mmiliki mpya na hivyo uongozi mpya,” akasema Lerner, na kuongeza kuwa Merrill Lynch wa Bank of America wameteuliwa kushauri kuhusu uuzaji.

“Ni wajibu wangu kwa Villa kusonga mbele, na kutafuta viongozi wapya na wenye msukumo, ikiwa nitahisi kwamba siwezi tena kuendelea na kazi,” akaongeza.


Bei ya chini kabisa inatarajiwa kuwa kati ya pauni 150-200 milioni($250-335 million) na shughuli ya uuzaji itageza kiwango cha njaa miongoni mwa wawekezaji kwa klabu za kati kwenye jedwali ya Ligi ya Premia.

Kulikuwa na uvumi kwenye tovuti za kijamii kwamba bilionea anayemiliki Oracle Larry Ellison angenunua klabu hiyo lakini kupewa majukumu kwa benki hiyo kunaonyesha kwamba Lerner anataka kusaka mnunuzi kutoka kote.

Villa, ambao ngome yao ni jiji la Birmingham, walimaliza nambari 15 katika Ligi ya Premia yenye timu 20 baada ya mechi za mwisho Jumapili.

Klabu hiyo ilipoteza zaidi ya pauni 50 milioni 2012-13 lakini ilisema hali yake ya kifedha iliimarika miaka iliyofuata kwani sasa Ligi ya Premia inajivunia mikataba mipya minono ya runinga.
Klabu hiyo inakadiria kupata mapato ya takriban pauni 116 milioni kwa mwaka utakaomalizika Mei 2014 na faida ya takriban pauni 17 milioni.

Villa have wameshinda taji la Uingereza mara saba lakini mara ya mwisho ilikuwa 1981. Walishinda Kombe la Ulaya msimu uliofuata na kikombe chao cha mwisho kikuu kushinda kilikuwa League Cup mwaka 1996.

Lerner ni mmoja wa Wamarekani kadha wanaomiliki klabu za soka za Ligi ya Premia.
Wawekezaji kama vile familia ya Glazer inayomiliki Manchester United, Stan Kroenke wa Arsenal na John W. Henry wa Liverpool wamevutiwa na uwezo wa Ligi hiyo wa kuzalisha pesa kupitia televisheni na uungwaji mkono wa mashabiki kutoka kila pembe ya dunia.

Hata hivyo, Fulham, inayomilikiwa na mfanyabiashara Mwamerika Shahid Khan, imeshushwa ngazi majuzi kutoka Ligi ya Premia na italazimika kutosheka na mapato ya chini ya ligi ya daraja la pili.