come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

WAJUMBE TFF WAPANIA KUMLIZA TENGA LEO, NJAMA ZA KUMNG'OA ANGETILE ZAJULIKANA

HUENDA leo hali ikabadilika katika mkutano mkuu maalumu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambako baadhi ya wajumbe wamepanga kufanya uamuzi mgumu wa kumuondoa madarakani Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Angetile Osiah, kwa madai ya kukosa imani katika utendaji kazi wake.


Mkutano wa leo ni maalumu kwa ajili ya kufanya marekebisho ya katiba ya TFF, unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa NSSF Waterfront, Dar es Salaam.

Baadhi ya wajumbe hao ambao hawakutaka kuandikwa majina yao kwa madai kuwa bado ni siri ya wajumbe wote, walidai uamuzi huo wa kumuondoa Osiah unaungwa mkono na wajumbe wengi, kwa madai anaiyumbisha TFF, akiwa kama mtendaji mkuu.

Mtoa habari huyo alisema wameazimia kukubali kupitisha katiba, licha ya kuwa kuna baadhi ya vitu lazima wavipatie ufumbuzi ili mambo yaweze kwenda sawa.

“Tunaweza kuwalaumu viongozi wengine TFF, ila sio wao, mambo mengi yanavurugwa na Osiah na kesho tutahakikisha tunamwondoa, kwani utendaji umemshinda,” alisema mtoa habari huyo.

Taarifa iliyotolewa juzi na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, inaeleza kuwa mkutano huo wa marekebisho ya katiba, utakuwa chini ya uenyekiti wa rais wa shirikisho hilo, Leodegar Tenga, kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Wambura alisema kila kitu kimekamilika, ikiwa ni pamoja na wajumbe wote wa mkutano huo kuwasili na wamefikia hoteli ya Travertine iliyoko Magomeni.

Alisema mkutano huo wa siku moja ukimalizika mapema, wajumbe wanaweza kuhudhuria mchezo wa kimataifa kati ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Uganda ‘The Cranes’ unaopigwa leo na ikishindikana, mkutano ni muhimu kuliko mechi, kwa kuwa mpira upo kila siku.

Pia, mkutano huo utahudhuriwa na wageni mbalimbali waalikwa wakiwemo kutoka Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA).


Aliongeza kuwa The Cranes ina kiwango kama Stars na kuwataka wachezaji kutohofia majina na kufanya kazi moja tu ya kusakata kabumbu.

Wakizungumzia mchezo huo, Kocha Kim wa Stars na Sredojvic Milutin ‘Micho’, kila mmoja alijinadi kushinda kutokana na maandalizi ambayo kila timu imeyafanya.

Kim alisema anamshukuru Mungu kikosi chake kutokuwa na majeruhi huku akiamini kushinda mchezo huo na kucheza fainali hizo, huku akiwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi na kuwapa sapoti kama ya mchezo uliopita dhidi ya Ivory Coast, licha ya kupoteza mchezo huo.

“Nina imani mchezo wa kesho utakuwa mzuri, nawaomba sana mashabiki waje watusapoti uwanjani na pia nampongeza Micho kwa timu yake kuwa katika nafasi nzuri kwenye viwango vya FIFA na nakubali ni wazuri, ila hata mimi nimejipanga kuwakabili,” alisema Kim.

Naye Micho alikiri kuwepo kwa vipaji vya soka hapa nchini na hiyo ndio sababu inayompa hofu katika mchezo wa leo, licha ya kuwa na uzoefu mkubwa katika ufundishaji wake, huku akisema lolote linaweza kutokea katika mchezo huo.

Micho aliyefuatana na nahodha wake Hassan Wasswa, alisema Stars imekuwa ikifanya vizuri tangu iwe chini ya Kim na itakuwa na wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza kinachocheza mechi za mchujo za Kombe la Dunia, wakati kwa upande wake atakuwa na wawili tu.

Katika hatua nyingine, jana jioni nusura litokee kasheshe Uwanja wa Taifa wakati timu hizo zilipokwenda kufanya mazoezi kwa nyakati.

The Cranes ambao walikuwa wamepangiwa kufanya mazoezi kuanzia saa 9:00 alasiri hadi 10 jioni kisha kuwapisha Taifa Stars, waligoma kufanya hivyo na kuibua rabsha miongoni mwa timu hizo mbili, huku Waganda wakitaka wagawane uwanja nusu kwa nusu.

Lakini hatimaye, makocha Milutin Micho na Kim Poulsen walitumia busara ya mazungumzo na hatimaye Waganda wakakubali kuondoka uwanjani kuwapisha Taifa Stars.