MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Boniventure Kabobo ‘Stamina’ anatarajiwa kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Jamvi la Wageni’ hivi karibuni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Stamina alisema katika wimbo huo ameshirikiana na mkali wa muziki huo Richard Martin ‘Rich Mavoko’ na ana imani utafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
“Nashukuru nyimbo zangu kukubalika na wadau mbalimbali, ambao wananipa msukumo wa kutunga mashairi yangu kwa utulivu na umakini mkubwa, hivyo wakae tayari kwa ajili ya kuipokea ngoma hii,” alisema Stamina.
Alisema anaamini mashabiki wanaozikubali kazi zake zinazoendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio watakuwa makini kusubiri ngoma hiyo mpya.
Msanii huyo alishatoa nyimbo kadhaa ambazo zinaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga zikiwemo, ‘Alisema’, ‘Kabwela’ na ‘Ushauri Nasaha’.