come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

JIMMY MPONDA AZUA JAMBO SOKONI KARIAKOO

Na Mtemi Msovela

Msanii wa filamu za mapambano, Jimmy Mponda, juzi Ijumaa alizua jambo kwenye kampuni moja ya kusambaza filamu baada ya kuelezea kuwa mpambanaji aliyecheza naye katika filamu mpya ya Doble J Final,ni pacha wake na si kweli kuwa kompyuta ndio ilitumika kutengeneza watu wawili waliofanana kama walivyofanya wasanii wakubwa wa Hollwood, Jean Cloud Van Dame na wengine.

"Huyo jamaa mwingine ambaye amefanana na mimi ni pacha wangu, yeye yupo nje huko na aliingia nchini kwaajili ya kucheza hii filamu!" Alisema Jimmy Mponda maarufu kama J Plus au Jimmy Master, na kuwaacha watu waliokuwa wakitazama master ya filamu yake hiyo mpya midomo wazi kwa mshangao kutokana na kushindwa kuwatofautisha kati ya yeye Jimmy Mponda na huyo pacha wake kwa jinsi walivyorandana.

Aidha Jimmy mponda alisema kuwa kama ndugu yake huyo angekuwa mwizi, angeweza kwenda popote na kutumia jina lake kuchukua mali yoyote na kutimka nayo bila kushtukiwa.
Msanii huyo anayevuma katika anga la filamu za mapambano,amesema katika filamu zake anajitahidi kuwapa  kipaumbele wasanii wasio na majina ili kiuwajengea mazingira mazuri ya ajira kwao.

Ndani ya filamu yake hiyO mpya, J,plus amemshirikisha mzee Charles Magali na wengine wote ni wasanii wapya ambao ni matunda yake.
Hata hivyo ndani ya filamu hiyo mpya Jimmy Mponda na pacha wake ndio waliozua majadala kwa jinsi walivyofanana kama mtu mmoja aliyegawanyika.

"Aisee kama asingesema mwenyewe, hakuna mtu angejua kama huyu jamaa ni pacha wake..!" alisema mtu mwingine aliyekuwa akitazama Master ya filamu hiyo mpya inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.