LONDON, ENGLAND
JOSE Mourinho ambaye atawasili Chelsea Julai
Mosi, amedaiwa kuanza kusaka majina sita ya kuyasajili kwenye dirisha
la majira ya joto.
Habari zinasema kocha huyo ana orodha ya mabeki wawili, viungo wawili na washambuliaji wawili.
Mourinho ataondoka rasmi Real Madrid Juni 2 na
kuna habari kuwa huenda akatambulishwa kabla ya Julai. Licha ya kuwa na
majina hayo, kocha huyo pia amewataka wachezaji wakubwa wasaini nyongeza
ya mwaka mmoja kama walivyotakiwa kufanya na viongozi wa juu.
Kocha huyo amebainisha kuwa timu nzuri ni ile yenye mchanganyiko wa wakongwe na vijana.
Imefahamika kuwa baadhi ya majina makubwa kwenye
orodha ya kocha huyo ni Radamel Falcao wa Atletico Madrid, kiungo wa
Malaga, Isco, nyota wa Everton, Marouane Fellaini na beki wa Porto,
Eliquim Mangala.
Lakini viongozi wa sasa wa Chelsea wapo katika
hatua nzuri ya kumsajili mshambuliaji wa Bayern Leverkusen, Andre
Schurrle na Mourinho amewataka wamrudishe kipa, Thibaut Courtois ambaye
yupo Atletico kwa mkopo wa muda mrefu.