come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

PATA MAKALA YA DIDIER KAVUMBAGU

Na Shaaban Kipresha

TAYARI alishaanza kupigiwa hesabu za kukatishiwa mkataba wake kama ilivyokuwa kwa nyota wengine wa kigeni ambao walishindwa kutimiza malengo ya Yanga.


Huko nyuma Yanga iliwahi kukatisha mikataba ya wachezaji wake wa kigeni waliosajiliwa kwa mbwembwe nyingi, Nani atakayemsahau Kenneth Asamoah Mghana aliyesajiliwa kwa madaha makubwa.

Ukimwondoa Asamoah, Davies Mwape Mzambia aliyetokea kuwa kipenzi cha Wanajangwani, Lakini wote hao walipoonekana kushindwa kukidhi kiu ya Wanajangwani walitupiwa virago vyao kwa aibu kubwa.

Ndivyo ilivyotaka kutokea kwa Mrundi Didier Kavumbagu ambaye kama si klabu ya Simba basi angekalia kuti kavu na huenda angeungana na akina Asamoah.

Kavumbagu alianza kung'ara na klabu ya Athletic ya Burundi ambayo ilikuja hapa nchini kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati mwanzoni mwa mwaka jana.

Yanga waliamua kuvunja benki na kumsajili mshambuliaji huyo aliyejengeka kimichezo baada ya kuonyesha makali yake katika michuano hiyo.

Kavumbagu alikuwa mmoja kati ya washambuliaji hatari waliotikisa katika michuano hiyo akiungana na Hamis Kiiza na Said Bahanuzi wa Yanga ambao walikuja kuibuka kuwa wafungaji bora kwani kila mmoja alifunga magoli sita.

Sifa kubwa iliyomfanya Kavumbagu asajiliwe na Yanga ni umahiri wake wa kufumania nyavu ambapo katika mchezo uliozikutanisha Yanga na timu ya straika huyo ya Athletic, Yanga ililala 2-0.

Magoli yote mawili ya Athletic yaliwekwa kimiani na Mrundi huyo, Ushindi huo wa Athletic uliwachanganya sana Yanga kwani walikuwa katika maandalizi mazuri ya kutetea taji lao.

Kavumbagu alionekana mwiba mchungu kwa mabeki wa Yanga ambapo aliweza kuwatoka na kuwanyanyasa mabeki visiki Kelvin Yondan na Nadir Haroub Alli 'Cannavaro' ambao walikuwa na kazi kubwa kumdhibiti mshambuliaji huyo.

Mashabiki wa Yanga walishindwa kuamini kuona kikosi chao kinazama uwanja wa Taifa huku Kavumbagu akiugusa mpira mayowe usikika kutoka kwa mashabiki wa Simba ambao kawaida yao kuizomea Yanga inaponyanyaswa.

Hata hivyo Yanga ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Kagame huku timu ya Kavumbagu ikiishia robo fainali, Baadaye Kavumbagu alikubali kumwaga wino Yanga na alipewa mkataba wa miaka miwili.

Kutua kwake Yanga kuliongeza hamasa kwa Wanajangwani hasa ukizingatia kiwango kilichoonyeshwa na mshambuliaji huyo katika michuano ya kombe la Kagame, Alianza kuitumikia Yanga katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Kavumbagu alionyesha ushirikiano mkubwa katika mechi zake za mwanzo na kufanikiwa kuongoza kwenye orodha ya wafungaji bora wa lkigi hiyo akichuana vikali na mshambuliaji wa Azam FC Kipre Tchetche anayetokea Ivory Coast.

Kavumbagu aliweza kufunga magoli tisa katika mzunguko wa kwanza na kuzidiwa goli na moja na Tchetche, Nyota huyo alianza kuhisi hujuma dhidi yake pale timu hiyo ya Yanga ilipofanya ziara yake nchini Uturuki.

Kasi yake ya kupachika magoli ilianza klupungua na kujikuta akishindwa kufunga na kuanza kushuka thamani, Jerry Tegete alianza kung'ara na ikafikia hatua sasa baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti ya michezo (Isipokuwa Kabumbu) yalianza kuripoti kuwepo kwa vitendo vya kishirikina ndani ya klabu ya Yanga.

Na aliyekuwa akifanya ushirikina huo si mwingine ni mshambuliaji Jerry Tegete, Baadaye ukawa ni mzozo mkubwa kati ya washambuliaji hao wawili na ndipo Yanga ilipoanza kupoteza mwelekeo katika safu ya ushambuliaji.

Washambuliaji wake wanne wote wakawa hawafungi huku Haruna Niyonzima, Nadir Haroub 'Cannavaro', Nizar Khalfan na Mbuyu Twite wakigeuka wafungaji katika mechi muhimu.

Mpaka ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara inafikia ukingoni bado Didier Kavumbagu alikuwa hajafanikiwa kufunga hata goli moja katika mzunguko huo wa pili, Uongozi wa Yanga pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Mholanzi Ernie Brandts lilianza kumpigia hesabu Mrundi huyo kumtema mara baada ya ligi kumalizika.

Kavumbagu angetemwa katika usajili ujao wa Yanga kutokana na kushuka kwa kiwango chake, Lakini alipewa mechi ya mwisho dhidi ya mtani wao wa jadi Simba iliyopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Yanga ambayo ilishatangaza ubingwa ikiwa na mechi mbili mkononi ilifanikiwa kusheherekea vema ubingwa wake baada ya kuilaza Simba mabao 2-0, Magoli ya Yanga yaliwekwa kimiani na Kavumbagu wakati lingine likifungwa na Hamis Kiiza.

Hii ni sawa kwamba bila ya Simba kumpa heshima ile basi angekuwa tayari analia kilio kama kile kilichowakuta akina Njoroge, Shikokoti, Ambani au Mwape ambao walikuja kwa mbwembwe Yanga na waliondoka kwa huzuni Yanga