Aliipoteza Simba uwanjani, Amuomba Poulsen amuite Stars
Na Shaaban Kipresha
INGAWA imevumishwa kuwa Simba ndio timu pekee inayoundwa na vijana wadogo wenye umri wa miaka 17 au 18 na kuitwa watoto na ilipokabiliana na Yanga, Mashabiki wa timu hiyo walitokea kuibeza Yanga na kuwaita wazee.
Waliamini Yanga imejaa wakongwe, Walidhani watashindwa kuchuana na damu changa ya Simba yenye yosso tupu, Lakini ukweli ulivyo kuwa Yanga ina yosso wengi kuliko Simba lakini haiandikwi hivyo.
Uwepo wake chipukizi Frank Domayo, Simon Msuva, Abdallah Mguhi 'Messi' na David Luhende sidhani kama kulipewa nafasi kuwa Yanga ina yosso kama ilivyo Simba.
Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Mholanzi Ernie Brandts na msaidizi wake Fred Felix Minziro imejaza yosso wengi wenye uzoefu wa kucheza soka la ushindani mahari popote duniani.
David Luhende mlinzi wa kushoto wa Yanga aliyeonyesha umahiri wa hali ya juu katika pambano la watani wa jadi Simba na Yanga lililochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katika mchezo huo wa watani ambao uliweza kukumbusha historia ya mwaka 1974 ambapo miamba hiyo ilikutana katika mchezo wa fainali ya ligi ya Taifa sasa ligi kuu katika uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza (sasa jiji).
Katika mchezo huo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutwaa ubingwa wa bara, Pia pambano hilo liliandika rekodi ya aina yake na ilikuja kuvunjwa kwenye pambano la hivi karibuni ambalo tulishuhudia Yanga ikiilaza Simba 2-0.
Sina shaka kikosi cha Yanga kilikuwa na kila aina ya dalili za kuibuka na ushindi kuanzia mashabiki hadi wachezaji, Yanga ilionekana itashinda mechi ile kutokana na maandalizi yake kufanywa kisasa na kitaalamu zaidi.
Kwa naza ilikwenda kuweka kambi yake visiwani Zanzibar na ilichagua sehemu sahihi ya kupumzika na kuifanya kambi yake, Mji wa Pemba wenye uwanja bora kabisa kwa sasa wa Gombani ulikuwa na kila aina ya kuifanya Yanga iibuke a usindi.
Tofauti na Simba ambao walikwenda kuweka kambi yao katika mji wa Unguja na waliutumia uwanja wa Mao Tsung, Yanga ilionyesha kuwa inaweza kuifunga Simba tena magoli mengi huku Simba ikipoteza muda kwa kusema hatufungwi tano na kikosi chetu cha watoto.
Walijua kabisa kuwa hawana uzoefu kwanini waliwafukuza wenye uzoefu, Lakini hilo halikuwapa Yanga kiburi na waliweza kukutana na changamoto nyingien kama zile za kuitwa wazee.
Siku ya siku ilipofika, David Luhende alikaa upande wa kushoto na alikumbana na mshambuliaji chipukizi wa Simba Haruna Chanongo.
Nani aliyebahatika kumuona Chanongo akifanya vitu vyake alivyovizoea kufanya katika mechi nyinginre zilizomfanya mpaka aitwe kwenye timu ya taifa, Taifa Stars.
Luhende aliamdhibiti vilivyo Chanongo na kumpoteza kabisa uwanjani, Kwa kifupi nyota huyo wa Yanga aliipoteza Simba katika mchezo huo na kusaidia kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Simba.
Magoli mawili ya Yanga yalianzia kwa Luhende ambaye alikuwa na kazi moja kuhakikisha washambuliaji wa Yanga wanafika langoni mwa Simba kupeleka kashikashi nyingi kwa kipa nambari moja wa Simba na timu ya taifa.
Chanongo alitolewa na kocha wa Simba Mfaransa Patrick Liewig baada ya kushindwa kuwafurahisha mashabiki wa Simba, Na wengi walidhani kuwa Yanga ilifanya hujuma kwa nyota wake ambao walishindwa kabisa kucheza soka la uhakika katika mechi hiyo.
Kiwango kilichoonyeshwa na Luhende katika mchezo huo kiliwashawishi wengi hata wakiwemo mashabiki wa Simba ambao walithubutu kumkubali nyota huyo na kumtaka kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars Kim Poulsen kumjumuhisha kijana huyo.
Pia wameishawishi klabu yao ya Simba kutafuta chipukizi wenye uwezo kama wa Luhende na kuchana na chipukizi wenye kutaka sifa na umaarufu katika kikosi cha Simba.
Akizungumza na Kabumbu, Lihunde alisema kuwa anamuomba mwalimu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen kumuangalia ili amjumuhishe, 'Nilikuwemo katika kikosi cha timu ya taifa iliyokuwa chini ya Jan Poulsen kipindi hicho naitumikia Kagera Sugar pamoja na ile ya vijana ya Kim', alisema Luhende.
Akizungumzia michuano ya Kagame inayofanyika nchini Sudan hivi karibuni, Lihende amesema Yanga ina nafasi kubwa kutetea taji lake.
'Katika misimu iliyopita ambapo Yanga ilitwaa ubingwa, Sisis wengine hatukuwa katika kikosi cha kwanza, Hivyo basi tunataka heshima yetu na tutajituma kwa hali na mali kuhakikisha tunarejesha kombe katika ardhi ya Tanzania', aliongeza Luhende.
Aidha Luhende amewataka mashabiki wa Yanga kumpa muda zaidi ili aweze kufanya mambo makubwa katika kikosi hicho, Je Luhende atafanya nini!, Basi ni jambo la kusubiri kisha tuone
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba 0755 522216, Toa maoni yako kuhusu David Luhende, Je wiki ijayo tumuanike nani kati ya Alli Mustapha 'Barthez' au Didier Kavumbagu