WAKATI Haruna Niyonziam
akiwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, habari zilizotufikia
hivi punde zinasema kiungo wa Simba, Amri Kiemba amesajiliwa na Yanga tayari
kwa kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.
Akizungumza na mtandao
huu, mtu mmoja kutoka kamati ya usajili ya Yanga, amesema Kiemba amesajiliwa kwa
mkataba wa miaka miwili ili kuongoza nguvu katika safu ya usajili ya Yanga.
Mtandao huu unaahidi kuwasiliana
na Kiemba muda mfupi atakapotoka mazoezini katika kambi ya Taifa Stars
kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2014.
Atakapotoka mazoezini mtandao
huu utawasiliana naye kiungo huyo ili aweze kueleza ukweli juu ya usajili wake
kwa Yanga.
Kiemba aliwahi
kuichezea Yanga miaka ya nyuma kabla ya kutimka katika timu hiyo.