come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MAMBO YAMEMNYOOKEA STEVE RNB

BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Music’, mkali wa muziki wa bongo fleva nchini, Steve RnB, anatarajia kuachia ‘singo’ mpya inayokwenda kwa jina la ‘Huyu Demu’ hivi karibuni.


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mkali huyo alisema katika kazi hiyo kamshirikisha nyota wa muziki huo, Mr. Blue na kwamba ameamua kutoa kazi hiyo mpya ili kuendelea kuwapa raha mashabiki wake, ambao wamekuwa wakimuunga mkono.

Alisema anayo matumaini makubwa ya wimbo huo kufanya vema katika medani ya muziki wa Bongo fleva, kama ilivyokuwa kwenye nyimbo zake zilizotangulia.

“Nawashukuru mashabiki kwa kuniunga mkono kwenye kazi zangu, sina cha kuwalipa zaidi ya kuwatayarishia kazi nzuri zaidi ambazo zitawaburudisha na kuwapa mafunzo ndani yake,” alisema.

Steve alipata kutoa singo matata ikiwamo ya ‘One Love’ alioimba na Baby Boy, ‘Jambo Jambo’ na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo