BAADA ya msanii Madee wa kundi la Tip Top Connection kutoka na wimbo wa 'Nani kamwaga pombe yangu' na kushika chati, Hatimaye nyota mwingine wa muziki wa kizazi kipya ameibuka na wimbo wa 'Chukua pombe yangu' ikiwa kama kumjibu Madee.
Akizungumza na mambouwanjani.blogspot.com leo hii, Msanii Salum Rashid au Dallarz kama anavyofahamika na mashabiki wake ametamba kuuachia wimbo huo hivi karibuni.
Dallarz amesema kuwa mbali ya kumjibu Madee, Lakini yeye ndiye mwanzilishi wa nyimbo za pombe ila Madee alichokifanya kubadilisha tu mashairi ya wimbo wake wa kwanza ;Sikosoba' ambao ulikuwa na ujumbe mzito.
Ameongeza kuwa Madee alikuwepo katika shoo yake iliyofanyika katika ukumbi wa Da West uliopo Tabata ambapo yeye aliuimba wimbo wa Sikosoba.
'Madee ni mjanja sana alichokifanya yeye ni kuchukua mashairi ya wimbo wangu wa Sikosoba na kuyaweka katika wimbo wake wa 'Nani kamwaga pombe yangu', alisema Dallarz, Hivyo wimbo wake huo unaanzisha malumbano mapya ya kugombea wimbo kati ya wasanii hao wawili.
Hata hivyo Dallarz amesema ana chuki na Madee ila alichofanya ni usanii tu, Lakini yeye ni tejiri wa mashairi na ameamua kumpa pombe yake ambayo Madee analalamika imemwagwa, Dallars pichani juu, Madee pichani chini