Katibu Mkuu wa Zamani wa Simba,
Mwina Kaduguda amemtaja kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima ndiye
mchezaji wa kigeni mwenye hadhi ya mchezaji wa kulipwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaduguda
alisema kuwa, amefuwafuatilia kwa karibu wachezaji wa kigeni wanaocheza
soka la kulipwa hapa nchini na kubaini wengi viwango vyao ni vya kawaida
vinavyofanana na wazawa.
“Tunatakiwa kuwa makini sana katika usajili
wetu, ukiniuliza mchezaji gani wa kigeni aliyeonyesha utofauti kwa kuwa
na kiwango cha juu pengine kuliko wa kwetu ni Niyonzima.
“Hakika huyu unaweza ukasema kwa hapa kwetu
inaweza kuchukua muda kidogo ili tupate mchezaji wa aina yake, lakini
hawa waliobaki unaweza kuwapata Manzese, Mwananyama kama ukiamua
kuwatafuta,” alisema Kaduguda.
Kaduguda ambaye pia aliwahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wakilichowahi kuwa Chama
Cha Soka Tanzania (FAT) alizitaka timu ziwe makini wakati wa kufanya
usajili wa wachezaji wa kigeni badala ya kukurupa na kuishia kuwalipa
fedha nyingi huku mchango wao dimbani ukiwa hafifu.
“Klabu ziwe makini, ziache kukurupuka na
kusajili wachezaji bomu, mchango wa Niyonzima kwa Yanga kila mmoja
ameuona, tunataka wachezaji wa namna hii,”.alisema Kaduguda.
Niyonzima amekuwa mchezaji tegemeo katika
kikosi cha Yanga tangu alipojiunga nayo misimu miwili iliyopita akitokea
APR ya Rwanda