Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel, imezindua msimu mpya wa
shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search, mwaka huu ikiwa imejipanga
kuwapa vijana wengi zaidi fursa ya kuonyesha na kuendeleza vipaji vyao.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark
Production, Rita Paulsen msimu huu wa saba toka shindano hilo lianzishwe
mwaka 2006, kuna vitu vingi vipya ikiwamo ongezeko la jaji mmoja ambaye
ni mdau wa muziki kutoka mkoa husika.
Naye Afisa Biashara mkuu wa Zantel, Sajid Khan
alisema uzinduzi huo ni furaha kwa kampuni hiyo kwani unaashiria
ufunguzi wa milango ya kuwasaidia vijana wengi wa Kitanzania kutimiza
ndoto zao.
“Mwaka jana pekee Epiq BSS ilifanikiwa kusaili
vijana zaidi ya elfu hamsini, jambo ambalo linaloonyesha kuna uhitaji wa
kuwekeza zaidi katika kuwaendeleza vijana’ alisema Khan.
Katika kuwapa fursa vijana ambao hawatafikiwa na
majaji, Zantel kwa kushirikiana na Push Mobile watafungua laini za
kurekodi kwa simu.