MSHAMBULIAJI Lionel Messi amepiku rekodi ya Diego Maradona ya kufunga mabao katika timu ya taifa ya Argentina, baada ya jana usiku kufunga mabao matatu peke yake akiiwezesha nchi yake kuibwaga Guatemala 4-0 katika mchezo wa kirafiki.
Nyota huyo wa Barcelona sasa analingana
kwa mabao na Hernan Crespo, 35 kila mmoja lakini anazidiwa kwa mabao 21
na gwiji Gabriel Batistuta.
Watu wamekuwa wakibishana sana juu ya
uwezo wa Messi na Maradona kwamba nani zaidi kati yao, lakini nyota wa
Barca akiwa na umri wa miaka 25 tu anaonyesha anaweza kustaafu akiwa
mfungaji bora wa kihistoria kwa nchi yake.
Amepitwa: Diego Maradona ameifungia
mabao 34 Argentina na alikuwa anashika nafasi ya tatu katika orodha ya
wafungaji wa kihistoria
Utamchagua nani? Ubishani kwamba nani zaidi kati ya Messi (kulia) na Maradona (kushoto)
Alirejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuwekwa benchi katika mechi mbili zilizopita kutokana na kuwa majeruhi.
Alifunga bao la kwanza kwa shuti la
mbali, kabla ya kumtengenezea nafasi ya kufunga bao la pili Augusto
Fernandez kisha akafunga kwa penalti kufikisha idadi ya mabao ya
Maradona kabla ya mapema kipindi cha pili kufunga bao la kumpiku gwiji
huyo, akiunganisha pasi ya Ezequiel Lavezzi.
Batigol: Gabriel Batistuta ndiye
mfungaji bora wa kihistoria wa Argentina akiwa mbele ya Hernan Crespo
(chini) na sasa na Messi pia
Lakini kocha wa zamani wa ufiti wa
Argentina, Fernando Signorini ameonya kwamba Messi anaweza akawa hayuko
vizuri wakati wa Fainali za Kombe la Dunia mwakani kutokana na kutumika
sana.
"Kabla, Miaka ya 60 na 70, wachezaji
walikuwa wanacheza mechi 80 hadi 90 kwa mwaka, lakini (Messi), ni
nambari moja duniani, anacheza mechi zaidi ya 120 kama ukihesabu mechi
zake za Barcelona na timu ya taifa,"alisema na kunukuliwa na Marca.
"Messi amecheza miaka mitatu bila
kuumia, lakini miezi miwili na nusu iliyopita aliumia misuli kabla ya
Nusu Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich nchini
Ujerumani, na akawekwa benchi katika mchezo wa marudiano. Kisha akaumia
tena,"alisema.
Wasiwasi: Messi anaweza asiwe vizuri kwa asilimia 100 wakati wa Kombe la Dunia kwa sababu ya kutumika sana