Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Maktaba za
Video Tanzania, Richard Kalinga alisema hayo Ijumaa iliyopita kwamba
kuwekwa kwa nembo hiyo ya TRA itasababisha kazi ya kuwatafuta wanaoiba
kazi za wasanii kuwa rahisi.
Alisema hayo kwenye mkutano wa wadau wa filamu
ulioandaliwa kwa ajili ya kulinda haki za wasanii wa filamu dhidi ya
waharamia na kuifanya sekta hiyo kulipa kodi katika serikali.
Taasisi ya BEST-AC kwa kushirikiana Indigo –MTPC
na Media for Development International (MFDI) ndiyo walioitisha mkutano
kwa ajili ya kusaidia kuondokana na uharamia wa kazi za wasanii wa
filamu.
Kalinga alisema katika utaratibu huo, kazi za
filamu zitanunuliwa zikiwa na nembo ya TRA, “mnunuzi akiona mkanda wa
filamu anaotaka kuununua hauna nembo hiyo afahamu kwamba huo siyo
halisi.”
“Mteja akinunua filamu ya aina hiyo afahamu kwamba
haitakuwa bora kwa sababu itakuwa imetengenezwa kiholela na kodi ya
serikali wanaikwepa,” alisema Kalinga.