KLABU ya Arsenal imeendelea na harakati za kuwania saini ya mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez.
Arsene Wenger anaamini mchezaji huyo
mwenye kipaji kutoka Uruguay ataisaidia Arsenal katika Ligi Kuu ya
England na anataka kuvunja rekodi ya usajili ya klabu yake kwa kutoa
Pauni Milioni 40.
Dau la Pauni Milioni 40 linaweza kuwa
sawa kwa Suarez, lakini inafahamika Arsenal itatoa kwanza Pauni Milioni
35 na nyingine Milioni 7 saba watalipa kwa vipengele, maana yake hakuna
namna ambayo Liverpool watakubali.
Ofa ya mafungu: Luis Suarez yuko tayari kuondoka Liverpool kabla ya mwisho wa msimu
Ofa za awali za Pauni Milioni 30 na
Milioni 35 tayari zimepigwa chini na Liverpool, ambayo ilimnunua kwa
Pauni Milioni 22.7 Suarez Januari mwaka 2011, lakini Arsenal imemfanya
mchezaji chaguo la kwanza katika inayowahitaji baada ya jithada zao za
kumnasa Gonzalo Higuain kueleeka kukwama.
Rekodi ya Arsenal kusajili mchezaji kwa bei kubwa ni Januari mwaka 2009, ilipolipa Pauni Milioni 15 kumnunua Andrey Arshavin.