come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

AZAM FC KUTAFUTA JOHN BOKO MPYA AGOSTI 6

KLABU ya ligi kuu ya Azam FC imetangaza kufanyika kwa majaribio kwa wachezaji chipukizi wanaotaka kuichezea timu hiyo kwa siku za usoni kwenye uwanja wake wa Azam Complex uliopo Chamanzi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa uongozi wa timu hiyo umeweka utaratibu maalum ambapo umewetaka wazazi au walezi kugharamia nauli za mambo mengine ili kumwezesha mtoto kuwahi haraka na kujumuika na wenzake katika mazoezi hayo ya majaribio.
 
'Majaribio kwa Azam Academy sasa yatafanyika Agosti 6 kuanzia saa moja asubuhi. Wazazi na walezi tunashauriwa kuwagharamia watoto wetu nauli, chakula, malazi na vifaa vya michezo', iliongeza taharifa hiyo.

'Majaribio ni kwa siku moja tu na tunahitaji wachezaji walio chini ya umri wa miaka 15.... kama mchezaji ana miaka chini 17 na ana kipaji cha hali ya juu sana pia atapewa kipaumbele', iliendelea taharifa hiyo.

'Baada ya mchakato na kama kijana atafuzu kujiunga na Azam Academy Mzazi/Mlezi atajaza fomu maalum kwa niaba ya kijana wake, Wachezaji mzingatie kuja na vielelezo vya umri wenu, (Cheti cha kumaliza elimu ya Msingi na Cheti cha kuzaliwa) kwa pamoja

Ilisema taharifa hiyo iliyosambazwa kupitia ukurasa wa klabu hiyo wa facebook