come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

BADO NIPO NIPO YANGA-KIIZA

MSHAMBUALIAJI Hamis Kiiza (Pichani) ambaye ni raia wa Uganda amesema kuwa yeye bado anaendelea kuisubiria Yanga kutokana na kuwepo kwa maendeleo juu ya kuongeza kwake mkataba mpya utakaomfanya kuichezea timu huyo kwa miaka miwili ijayo.


Akizungumza na mtandao huu jana, Kiiza maedai kitendo cha kuja nchini na kuondoka kinatokana na kutokuwepo kwa kiongozi mmmoja wa Yanga aliye katika majukumu makubwa kwa sasa, Mussa Katabaro anasubiriwa ili aweze kumalizana na mchezaji huyo.

Kiiza maewataka wapenzi na mashabiki wa Yanga kuwa na imani naye kwani kinachotokea sasa ni muendelezo wa mazungumzo yao, Anasema hakuna ugumu wowote yeye kusaini mkataba mpya Yanga ila anasubiria mipango ikjamilike na atamwaga wino.

"Wakala wangu ameniambia mambo yote yako safi na niendelee kuwa na subira hivyo hakuna kitu kinachonikatisha tamaa', alisema Kiiza, Mashabiki wa Yanga bado wamejaa machungu hasa kufuatia kusikia habari zinazomuhusu mchezaji huyo kuwa hadi sasa hajasaini mkataba mpya.

Hivi karibuni Yanga iliamua kuachana na mchezaji huyo aliyeipa ubingwa wa ligi kuu pamoja na klabu bingwa Afrika mashariki na kati mwaka jana, Kiiza nafasi yake imekuwa ikiwaniwa na nyota kadhaa akiwemo Mnigeria Ogbu Brendan Chikwudi ambaye hata hivyo ametupiwa virago vyake na kurejea kwao