come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ULINZI YAILAZA CITY STARS



Ulinzi Stars walikwamilia nafasi ya tatu kwenye ligi baada ya ushindi muhimu wa 1-0 ugenini dhidi ya City Stars mnamo Jumamosi kwenye mechi iliyochezwa adhuhuri uwanjani Hope Centre.

Bao hilo la pekee lilifungwa dakika ya 82 na Kevin Amwayi na kuwapa wanajeshi hao ushindi wao wa pili katika mechi mbili. Mechi hiyo, hata hivyo, haikuwa na aliyetawala licha ya mchezo mzuri kutoka kwa mshambuliaji wa Ulinzi Evans Amwoka mara kadhaa.
City Stars, ambao hawakufanyia mabadiliko kikosi chao kutoka kwa kile kilichocheza wikendi iliyopita, hawakusalimu amri rahisi na walilinda kwa hali na mali kupitia walinzi wao Oliver Kiprutto, Hassan Mohammed na mchezaji wa zamani wa kimataifa Mulinge Ndetto.
Kutokuwepo kwa Jimmy Bageya katika kikosi cha wachezaji XI wa kwanza kulionekana hata hivyo huku City Stars wakihangaika safu yao ya mashambulizi nao walinzi wa Ulinzi wakiweka ukuta.
Kipindi cha pili mambo yalikuwa vilevile huku Ali akimwingiza mfungaji mabao mengi ligini wa zamani Steve Waruru kuchukua pahala pa Kelvin Simiyu. Hatua hii ilionekana kuwafaa wanajeshi kwani kiungo huyo wa kati mwenye kasi alikimbia mara kadha kulia na kuhangaisha sana walinzi wa City Stars.
Oscar Wamalwa baadaye aliingizwa, na kuacha washambuliaji wa City Stars wakiwa wamefungiwa kabisa huku kocha Ali akiamua kujilinda zaidi.
Bao la Amwayi dakika za mwisho za mechi hata hivyo liliwafanya Ulinzi wapumue kiasi, na baadaye wakafunga dirisha lao kabisa na kukwamilia alama hizo tatu.
Ulinzi sasa wamo nafasi ya tatu kwenye jedwali,wakisubiri mechi zitakazochezwa Jumapili adhuhuri.