come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

HUJUMA: KUUNGUA NYUMBA YA NIYONZIMA WEKUNDU WAHUSISHWA

Siku moja mara baada ya kuungua kwa nyuma ya mchezaji wa Yanga Haruna Niyonzima, kuna taarifa zinaeleza kuwa kulikuwa na njama kubwa zilizopangwa na baadhi ya mashabiki wanaodhaniwa kuwa wa Simba ili kuidhoofisha Yanga.


Hivi karibuni beki wa kutumainiwa wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani Mbuyu Twite kuibiwa vitu vyake vyote vya ndani na watu wasiojulikana lakini baadaye ikajulikana kuwa waliofanya wizi huo walikuwa mashabiki wa Simba.

Mtaa anaokaa Twite inasemekana wanaishi mashabiki wengi wa Simba kuliko wa Yanga ambao ni wachache, hivyo suala la UNiyonzima linahusishwa na njama za Simba ili kuidhoofisha Yanga ambayo inaonekana kumtegemea zaidi nyota huyo raia wa Rwanda