come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

TUTAIFUNGA SIMBA-CHUJI

Kiungo anayesifika kwa sasa nchini Athuman Idd 'Chuji' wa Yanga amefunguka na kusema kuwa wataifunga Simba katika mchezo wao wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ifikapo Oktoba 20 ambapo timu hizo zitakutana.


Akizungumza na Kabumbu Spoti jana wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Loyola Mabibo jijini Dar es Salaam jana amedai Yanga ina kikosi bora kuliko Simba ila amedai Simba wanasifika magazetini tu.

Chuji amesema Yanga ni timu ngumu na hata mechi zake za mwanzo imecheza na timu imara kuliko watani zao Simba ambao wamecheza na timu dhaifu, 'kikosi cha Yanga ni cha ushindi tofauti na Simba ambao wamejaa misifa tu magazetini', aliongeza Chuji.

Mpaka sasa Yanga inashika nafasi ya tano ikiwa imeachwa kwa tofauti ya pointi tano na Simba inayoongoza ligi kwa pointi 14, msimu uliopita Yanga ilianza ligi vibaya kwa tofauti ya pointi tisa lakini ikaja kuibuka mabingwa wa bara.

Kwa kauli ya Chuji inawezekana Yanga ikafanya kama msimu uliopita ambapo ilianza vibaya ligi na kumaliza vizuri, Yanga imejikuta ikianza ligi kwa ushindi dhidi ya Ashanti United wa mabao 5-1 lakini mechi zilizofuata ilitoka sare tatu mfululizo dhidi ya Coastal Union, Mbeya City, Prisons za kufungana mabao 1-1 kisha ikafungwa na Azam 3-2, na kuilaza Ruvu Shooting 1-0.