come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

CHELSEA WAONA MWEZI.........

MABAO mawili ya Ramires moja kila kipindi, moja la wenyeji kujifunga na moja la Frank Lampard yamempa furaha kocha Mreno, Jose Mourinho baada ya Chelsea kuichapa Steaua Bucharest mabao 4-0 katika Ligi ya Mabingwa usiku.


Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Ivanovic, Terry, Luiz, Cole, Ramires, Lampard, Oscar/Azpilicueta, Mata/Willian dk80, Schurrle na Torres/Eto'o dk11.

Steaua: Tatarusanu, Georgievski/Varela dk71, Szukala, Gardos, Latovlevici, Bouceanu, Filip, Popa/Kapetanos mapumziko, Stanciu, Tanase na Piovaccari/Tatu mapumziko.

Katika mchezo mwingine, bao pekee la Fabregas dakika ya 75 lilitosha kuipa ushindi wa ugenini, Barcelona wa 1-0 dhidi ya Celtic nchini Scotland.

Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra, Adriano, Xavi, Busquets, Iniesta, Fabregas/Tello dk78, Pedro/Sanchez dk74 na Neymar.
Celtic: Forster, Lustig/Forrest dk70, van Dijk, Ambrose, Izaguirre, Matthews, Brown, Mulgrew, Samaras, Commons/Pukki dk86, Stokes/Kayal dk70.

Katika mchezo mwingine, bao la dakika mwishoni mno la mkwaju wa penalti wa Mario Balotelli limeinsuru AC Milan kulala baada ya kupata sare ya 1-1 na Ajax katika Kundi H.

Waholanzi walifikiri wameshinda baada ya bao la kichwa la Stefano Denswil dakika ya 90, lakini kulikuwa kuna zali la Balotelli aliyechezewa rafu na Mike van der Hoorn kwenye eneo la hatari na mwenyewe akaenda kufunga kwa tuta..

Easy does it: Mario Balotelli was composed enough to roll in a late, late penalty for AC Milan at Ajax
Fungeni midomo yenu: Mario Balotelli akipongezwa na wenzake kwa kazi nzuri

Schalke inaongoza kundi E kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Basel, bao pekee la Julian Draxler dakika ya 54.

Washindi wa pili wa msimu uliopita, Borussia Dortmund walipata pointi zao za kwanza baada ya kuifunga Marseille ambayo haina pointi hadi sasa mabao 3-0.

Dortmund iliyofungwa na Napoli wiki mbili zilizopita, ilipata mabao yake kupitia kwa Robert Lewandowski dakika ya 19 na 79 kwa penalti na Marco Reus dakika saba baada ya kuanza kipindi cha pili.