Nyota huyo wa Manchester United, ambaye amebeba matumaini ya kocha Louis van Gaal kutwaa Kombe la Dunia, alikuwa amefungwa plasta ya kutosha katika mguu wake wa kushoto wakati wakiondoka kwenye kambi ya mazoezi ya Flamengo.
Uholanzi inamenyana na Costa Rica mjini Salvador katika Robo Fainali ya Kombe la Dunia Jumamosi na inamuhitaji van Persie kuwa fiti.