come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

DIANA KIMARO AMSHUKURU MUNGU KWA KUMJAALIA MIGUU YA BIA

Diana Kimaro kwa vituko hajambo !...new gossip kutoka kwa rafiki wa karibu na star huyo ni kuwa Diana huwa anajitapa kuwa na miguu ya bia yaani miguu minene yenye mvuto kwa madai mastaa wenzake wengi wa kike hawana.

Chanzo hicho kimesema kuwa Diana anavaa vimini na magauni mafupi muda wote sababu ya miguu hiyo ya bia aliyojaaliwa ikidaiwa wanaume wanadata nayo.

" Diana kila siku anajisifu kwa kuwa na miguu ya bia, yaani anamshukuru Mungu, kwani nyie mshawahi kumuona akivaa nguo ndefu? basi jibu ni hilo ana guu la kimini(huku akiangua kicheko), wanaume wengi wanamsifia ndo sababu vimini haachi" kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo Diana anayetamba sasa na filamu za Danija na Kigodoro hakuweza kupatikana kuzungumzia issue hiyo ya kuwa na miguu ya beer.

Mbali na msanii kujisifia mwenyewe ingawa kweli ameumbika, inasemekana anataka kupambanishwa na msanii mwenzakew Elizabeth Michael 'Lulu' ambaye naye anasifika kwa uzuri kama ilivyo kwa Diana.


Endapo nyota hao watapambanishwa na kuonekana mmoja mshindi ndio kutaweza kuamua nani zaidi ya mwenzake kwa sasa, nyota ya Diana inaonekana kung'ara kwa sasa ambapo amekuwa akitamba katika vichwa vya habari katika magazeti ya udaku pamoja na mitandao ya kijamii

Chanzo Swahiliworldplanet