come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

LAANA ZA YANGA ZAMTESA DOMAYO


KIUNGO wa zamani wa Yanga Frank Domayo ambaye alisajiliwa kwa mbwembwe nyingi na mabingwa wapya wa Tanzania bara Azam fc sasa atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa miezi minne hivyo ataukosa mzunguko wa kwanza unaotarajia kuanza mwezi ujao.

Kwa mujibu wa daktari wake, Domayo hatocheza soka tena kwa muda huo hivyo ataikosa mechi muhimu dhidi ya klabu yake ya zamani Yanga ambayo itachezwa mapema kabla ya ligi kuanza, mechi hiyo ya Ngao ya Hisani itachezwa wiki moja kabla ya ligi kuu bara kuanza.

Kukosa kwa mechi hizo Domayo kumesababishwa na majeruhi aliyonayo ambapo Azam wenyewe wanasema alikuwa nayo tangia akiwa Yanga, Lakini wadadisi wa mambo wanadai kuwa hizo ni laana kwa mchezaji huyo dhidi ya Yanga ambao ndio waliokuwa wanammiliki.


Yanga haikumtema Domayo isipokuwa Domayo aliitema Yanga, wenyewe walitaka kumuongezea mkataba mpya lakini akawachengachenga mpaka kusaini Azam kwa mkataba wa miaka miwili, bado alikuwa tegemeo kwa upande wa Yanga na Taifa Stars lakini aliondoka na kuwaacha Yanga vichwa chini.

Kupasuliwa kwake goti kunaashilia kuipisha mkono ligi kuu kwa muda na akiwa tayari kurejea anahitaji kupigania namba upya kwani kuna nyota wengine wanatafuta nafasi pia, kusajiliwa kwa Athuman Chuji na Azam huenda kukazima ndoto za kiungo huyo aliyeikwepa Yanga kwa makusudi.

Picha zote kwa hisani ya Bin Zubeiry Blog