come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

USAJILI ULAYA WAANZA KUPASUA VICHWA KLABU

Arsenal wameanza tena kumfuatilia kiungo wa Bayer Leverkusen Lars Bender, huku Arsene Wenger akiwa anakaribia kukamilisha usajili wa Alexis Sanchez na beki Mathew Debuchy (Daily Telegraph), Arsenal wamekubaliana na Barcelona pauni milioni 34 za kumsajili Sanchez, lakini Barca bado wanatazama kama Juventus wanaweza wakatoa dau kubwa zaidi.

Liverpool pia wanamtaka Sanchez, lakini mchezaji huyo hataki kwenda Anfield. Manchester United wameambiwa kuongeza dau kama wanamtaka beki Daryl Janmaat kutoka Feyenoord (Metro), Luis Nani atakuwa mtu muhimu wakati Man U wakimfuatilia Arturo Vidal wa Juventus (Evening News).


Southampton wanajiandaa kutoa pauni milioni 8 kumsajili kipa wa Cardiff David Marshall (Daily Mail), Louis van Gaal anapanga kutumia mkakati wa 3-4-3 anaotumia na Uholanzi wakati atakapoanza kuifundisha Man U (Daily Mirror), Monaco wanamtaka kiungo wa Newcastle Moussa Sissoko ambaye pia anasakwa na Liverpool (L'Equipe), Arsenal, Tottenham.

Napoli na Borussia Dortmund wote wanamwania kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin (L'Equipe), Manchester United na Paris St-Germain wapo tayari kutoa pauni milioni 47 kumsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria (AS.com).

Marouane Fellaini ambaye amekuwa na wakati mgumu Man U huenda akachukuliwa na Fiorentina (Lefigaro), Monaco wamewaambia Real Madrid kutoa pauni milioni 63 kama wanamtaka kiungo kutoka Colombia James Rodrigues (AS.com), mmiliki wa AC Milan Silvio Berlusconi ana wasiwasi kuwa hatopata bei anayotaka kwa Mario Balotelli kwa Arsenal kutokana na kutofanya vyema katika Kombe la Dunia.